Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis Tafsiri: Al-Baqarah Ayah 65

2:65
ولقد علمتم الذين اعتدوا منكم في السبت فقلنا لهم كونوا قردة خاسيين ٦٥
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعْتَدَوْا۟ مِنكُمْ فِى ٱلسَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا۟ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ ٦٥
وَلَقَدۡﱹ
عَلِمۡتُمُﱺ
ٱلَّذِينَﱻ
ٱعۡتَدَوۡاْﱼ
مِنكُمۡﱽ
فِيﱾ
ٱلسَّبۡتِﱿ
فَقُلۡنَاﲀ
لَهُمۡﲁ
كُونُواْﲂ
قِرَدَةًﲃ
خَٰسِـِٔينَﲄ
٦٥ﲅ
Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika mlijua, enyi kongamano la Mayahudi na Wanaswara, adhabu iliyowapata mababu zenu waliopita, watu wa kijiji kilichoasi amri ya Mwenyezi Mungu katika yale aliyowachukulia ahadi ya kuitukuza Siku ya Jumamosi. Wakafanya hila ya kuvua samaki siku ya Jumamosi kwa kuweka mitego na kufukua mashimo. Walipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu aliwageuza kuwa manyani wenye kudharauliwa.