Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis Tafsiri: Al-Furqan Ayah 23

25:23
وقدمنا الى ما عملوا من عمل فجعلناه هباء منثورا ٢٣
وَقَدِمْنَآ إِلَىٰ مَا عَمِلُوا۟ مِنْ عَمَلٍۢ فَجَعَلْنَـٰهُ هَبَآءًۭ مَّنثُورًا ٢٣
وَقَدِمۡنَآﱢ
إِلَىٰﱣ
مَاﱤ
عَمِلُواْﱥ
مِنۡﱦ
عَمَلٖﱧ
فَجَعَلۡنَٰهُﱨ
هَبَآءٗﱩ
مَّنثُورًاﱪ
٢٣ﱫ
Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hapo tutayaleta yale waliyoyafanya yanayoonekana kuwa ni mazuri na ya kidini, tuyafanye ni yenye kubatilika na kupotea. Hayatawanufaisha na yatakuwa ni kama vumbi linalorushwa, nalo ni lile vumbi lembamba linaloonekana kwenye mwangaza wa jua. Hivyo ni kwamba matendo mema hayawi na manufaa yoyote huko Akhera isipokuwa mwenye kuyafanya awe na imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtakasia na kumfuata Mtume Wake Muhammd, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.